Sisi Ni Nani
Sisi Ni Nani
UANZISHWAJI
Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) imeanzishwa chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Usalama wa Chakula, Sura 249, kwa marekebisho ya lazima (consequential amendment) ya Sheria hiyo. Marekebisho hayo yalifanyika kupitia Sheria ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Na. 19 ya mwaka 2009.
WAJIBU
COPRA imekabidhiwa mamlaka ya kudhibiti na kusimamia uzalishaji, uchakataji na masoko ya nafaka na mazao mchanganyiko, kwa kuhakikisha ubora, usalama na upatikanaji wa chakula kwa Tanzania na nje ya nchi.