Leo tarehe 26/08/2025, Watumishi wa COPRA – Nyanda za Juu Kusini wametembelea taasisi za kilimo ikiwemo TPHPA, TFRA na SAGCOT. Lengo la ziara hii lilikuwa kufahamiana, kubadilishana mawazo na uzoefu baina ya taasisi husika, pamoja na kujadili namna bora ya kushirikiana katika utekelezaji wa shughuli za pamoja (joint activities) kwa manufaa ya sekta ya kilimo.
Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Bishwadip Dey amekutana ametembelea Banda la Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo 2025 yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Tukutane Nane Nane 2025: Tembelea Banda la COPRA katika Ofisi za Kanda zilizopo nchini. “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025“
Leo tarehe 9 Julai, COPRA imesaini makubaliano ya kimkakati na Yas Business pamoja na MIXX by Yas, kwa lengo la kuimarisha matumizi ya mifumo ya kidigitali katika upatikanaji wa masoko, taarifa sahihi za bei ya mazao, malipo, na huduma nyingine za kifedha kwa wakulima na wadau katika mnyororo wa thamani wa mazao ya nafaka na mazao mchanganyiko.
Miongoni mwa viongozi waliotembelea banda la COPRA leo tarehe 7 Julai 2025 ni Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Dkt. Benson Ndiege. Viongozi mbalimbali na wanachi wanaendelea wametembelea banda la Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).
Rais mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, alipotembelea banda la COPRA akiwa ameambatana na Mhe. Waziri wa Viwanda na Biashara, Suleiman Jaffo, katika kuadhimisha sherehe za Sabasaba Jijini Dar es Salaam mwaka 2025.
Tarehe 13 Novemba, Mkurugenzi Mkuu wa COPRA, Irene Madeje Mlola, alishiriki katika kikao kuhusu “Sera za Biashara na Uwekezaji ili Kukuza Mipango ya Hali ya Hewa na Maendeleo Endelevu” katika Mkutano wa COP 29.
ZIARA YA HESHIMA KWA BANDA LA TANZANIA - FRUIT LOGISTICA, BERLIN, UJERUMANI – 6 FEBRUARI 2025.
Mhe. Hassani Iddi Mwamweta, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani (ambaye pia anawakilisha Tanzania katika Uswisi, Jamhuri ya Czech, Slovakia, Romania, Poland, Hungary, Bulgaria, na Vatican), alitembelea banda la Tanzania kwenye maonesho ya kimataifa ya Fruit Logistica nchini Ujerumani.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), Bi. Irene Mlola, mara baada ya kusaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) na taasisi ya Corus International kwa ajili ya kushirikiana katika kuendeleza tasnia ya zao la kakao tarehe 25 Aprili 2025
DAWATI LA HUDUMA KWA WATEJA - MAMLAKA YA UDHIBITI WA NAFAKA NA MAZAO MCHANGAYIKO
Tarehe 22 Machi, 2024, COPRA iliyowakilishwa na Afisa Mkuu wa Kilimo, Bi. Mary Majule, ilialikwa kuwa mgeni rasmi na kufungua Kongamano la Wadau la kumaliza mradi wa AINFP (Alliance for Inclusive and Nutritious Food Processing). Mradi huu ni ushirikiano kati ya Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), TechnoServe na Partners in Food Solutions(PFS).