Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), kwa kushirikiana na ASPIRES kupitia mradi wa Feed the Future Tanzania Kilimo Tija (KTA) na Wizara ya Kilimo kupitia Mradi wa Kuwezesha Upatikanaji wa Pembejeo za Kilimo Tanzania (TAISP), wakiwa Morogoro kwa ajili ya kupitia na kuboresha rasimu ya kanuni za Utekelezaji wa Sheria ya Usalama wa Chakula Sura 249 na marekebisho yaliyofanywa kupitia sheria ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Sura 274 - Novemba 2024
Shiriki kikamilifu na piga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024.
EUDR ni kifupi cha European Union Deforestation Regulation. Ni kanuni mpya iliyopitishwa na Umoja wa Ulaya (EU) yenye lengo la kupunguza athari za bidhaa zinazohusiana na ukataji wa misitu (deforestation) katika minyororo ya thamani ya biashara ya kimataifa. EUDR inalenga kuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingizwa au kuuzwa ndani ya soko la EU hazichangii ukataji wa misitu au uharibifu wa mazingira.
Mwelekeo wa Serikali ni kutumia Mifumo ya Stakabadhi Ghalani na TMX ili kumnufaisha mkulima na jasho lake na pia kupata takwimu sahihi za kilimo ili zisomeke kimataifa na Tanzania iweze kusonga mbele kwenye biashara ya Mazao yetu - Septemba 2024
Tarehe 13 Novemba, Mkurugenzi Mkuu wa COPRA, Bi. Irene M. Mlola, alishiriki kwenye kikao cha ‘Sera za Biashara na Uwekezaji kwa Maendeleo Endelevu na Kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi katika mkutano wa COP 29.
The Director General of COPRA, Irene Madeje Mlola, participated as a panelist in the launch of the "Growing Together" program in Dar es Salaam on 6 November 2024, where she discussed Tanzania’s pathways to increasing farmer productivity and beneficiation through market systems. COPRA is dedicated to establishing and strengthening market systems that promote transparency, elevate quality standards, and secure Tanzania's food supply
The Director General of COPRA, Irene Madeje Mlola, participated as a panelist in the launch of the "Growing Together" program in Dar es Salaam on 6 November 2024, where she discussed Tanzania’s pathways to increasing farmer productivity and beneficiation through market systems. COPRA is dedicated to establishing and strengthening market systems that promote transparency, elevate quality standards, and secure Tanzania's food supply
Mkutano wa Mashauriano ya Wadau kwa ajili ya Uthibitishaji wa Awali wa Mpango wa Pamoja wa Mbegu (JSAP) uliofanyika Morogoro tarehe 08 Novemba 2024.
Mkutano wa Tisa (9) wa Baraza la Pareto uliofanyika leo tarehe 6 Novemba 2024 Jijini Dodoma, ukilenga kujadili masuala muhimu ya bei kwa msimu wa 2024/2025.
Huu ni mojawapo ya maandalizi kabla ya Mkutano Mkuu wa Wadau (AGM) uliofanyika tarehe 7 Novemba 2024 kuanzia saa 3 asubuhi katika Hoteli ya Midlands, Dodoma. Tukio hili linatoa fursa kwa wadau kuchangia mawazo na kupata ufahamu kuhusu mwelekeo wa soko katika msimu ujao.
Wadau wa Pareto wakifuatilia mada na majadiliano katika Mkutano Mkuu wa 14 wa wadau wa Pareto uliofanyika tarehe 07 Novemba 2024 , Jijini Dodoma