Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Cereals and Other Produce Regulatory Authority

(COPRA)

COPRA Logo
"Commercialization of the Tanzania’s Food systems to catalyze growth and resilience"

CHONGOLO AZINDUA MIONGOZO MIPYA YA KUINUA UZALISHAJI WA UFUTA NA MAZAO YA MIKUNDE

Reason Image

Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, amezindua miongozo mipya ya uzalishaji endelevu wa mazao ya  ufuta, maharage, dengu, choroko, soya na mbaazi.

 

Uzinduzi wa miongozo hiyo ya mazao yanayosimamiwa na Mamlaka ya Uthibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), ulihudhuriwa na zaidi ya wataalam wa kilimo na ushirika 600 kutoka mkoa halmashauri zote za mkoa  wa Lindi.

 

 Waziri Chongolo alitumia fursa hiyo kusisitiza umuhimu wa miongozo hiyo katika kuboresha mnyororo wa thamani wa mazao na kuongeza tija kwa wakulima.

 

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa COPRA, Irene Mlola, amesema miongozo hiyo itakuwa nyenzo muhimu ya kuongeza uzalishaji na kukidhi mahitaji ya masoko ya kimataifa, hatua itakayoongeza kipato kwa wakulima na kuimarisha  biashara ya mazao ya kilimo.

 

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Rajab Telack, aliwataka watumishi wa umma katika mkoa huo kujishughulisha na shughuli za kilimo kwa ajili ya kujiongezea kipato.

 

Aidha Maafisa Kilimo na Ushirika walipongeza hatua hiyo, wakieleza kuwa miongozo hiyo itawawezesha kusimamia vyema uzalishaji kwenye maeneo yao ya kazi na kuwawezesha wakulima kuzalisha mazao yenye ubora kwa kuzingatia mahitaji ya soko.