COPRA YAGAWA TANI 7 ZA MBEGU KWA WAKULIMA LINDI
COPRA YAGAWA TANI 7 ZA MBEGU KWA WAKULIMA LINDI
Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) imeendelea na zoezi la kugawa mbegu bora kwa wakulima na sasa imewafikia wakulima wa zao la ufuta katika Mkoa wa Lindi na kukabidhi jumla ya tani saba za mbegu ya ufuta. Mkurugenzi Mkuu wa COPRA, Bi. Irene Mlola amemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Victoria Mwanziva aliyepokea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Terak.
