Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Cereals and Other Produce Regulatory Authority

(COPRA)

COPRA Logo
"Commercialization of the Tanzania’s Food systems to catalyze growth and resilience"

WAZIRI CHONGOLO AIPONGEZA COPRA

Reason Image

Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo, ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) kwa utekelezaji madhubuti wa majukumu yake katika kipindi cha miaka miwili tangu kuanza rasmi kwa oparesheni zake. Pongezi hizo zilitolewa wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha wataalamu wa COPRA wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bi. Irene. Mlola, Wizara ya Kilimo na taasisi mbalimbali za serikali, kikiongozwa na Mhe. Waziri mwenyewe.

Akiwasilisha maelekezo ya wizara, Mhe. Chongolo aliitaka COPRA kupanua wigo wa usimamizi na udhibiti wa mazao ya kimkakati, hususan yale yanayoongeza kipato kwa mkulima na kuchochea ukuaji wa Uchumi wa Taifa. Alisema kuwa mazao kama karafuu na kakao yana soko la uhakika ndani na nje ya nchi, hivyo ni muhimu kuyawekea mifumo madhubuti ya uzalishaji na uwezeshaji.

“Kuna mazao kama karafuu na kakao ambayo tayari yana uhakika wa masoko, hivyo ni lazima tuyafanyie kazi na kuweka mifumo sahihi, ikiwemo kutoa miche bora kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji nchini,” alisema.

Katika hatua nyingine, Mhe. Waziri alimuelekeza Mkurugenzi Mkuu wa COPRA, Bi. Irene Mlola, kuhakikisha kunakuwepo na mipango ya muda mfupi na muda mrefu inayolenga kutekeleza Ajenda 10/30, hususan katika kupunguza utegemezi wa uagizaji wa mazao muhimu kama chikichi na ngano. Alisisitiza kuwa mipango hiyo inapaswa kuendana na dira ya kuongeza uzalishaji wa ndani na kuimarisha usalama wa chakula nchini.