Kikao cha ‘Sera za Biashara na Uwekezaji kwa Maendeleo Endelevu na Kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi katika mkutano wa COP 29 - Tarehe 13 Novemba 2024
Tarehe 13 Novemba, Mkurugenzi Mkuu wa COPRA, Bi. Irene M. Mlola, alishiriki kwenye kikao cha ‘Sera za Biashara na Uwekezaji kwa Maendeleo Endelevu na Kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi [Trade and Investment Policies to Advance Climate Ambition and Sustainable Development]’ katika mkutano wa COP 29.
Katika kikao hicho, Bi. Mlola alielezea juhudi za Tanzania kupitia COPRA katika kuimarisha mifumo rasmi ya masoko kwa mazao yenye thamani kubwa yanayoongoza kwenye soko la nje. Lengo kuu ni kuhakikisha upatikanaji wa haki kwenye masoko na kugawana mapato kwa usawa kwa wadau wote wa mnyororo wa thamani, hususan wakulima. Mbinu hii inasaidia kuimarisha ustawi wenye uvumilivu na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kutokomeza umaskini, ambao ni moja ya chanzo kikubwa cha uharibifu wa mazingira.