Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Cereals and Other Produce Regulatory Authority

(COPRA)

COPRA Logo
"Commercialization of the Tanzania’s Food systems to catalyze growth and resilience"

Usajili wa Wadau wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko Kuanzia Januari 2025

Reason Image

27 Desemba, 2024

TANGAZO KWA UMMA

 USAJILI WA WADAU WA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO KUANZIA JANUARI 2025

  1. Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) inapenda kuwatangazia Wadau wote waliopo kwenye mnyororo wa mazao yote yanayosimamiwa na Mamlaka, hususan: Wanunuzi (Buyers), Wauzaji (Sellers), Wachakataji (Processors), Waingizaji ndani ya nchi (Importers) Wasafirishaji nje ya nchi (Exporters), Wasafirishaji ndani ya nchi (Transporters) na Wasafishaji (Produce Cleaning Center) wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko kuwa wanatakiwa kujisajili kuanzia Januari 2025 ili waweze kutambulika rasmi na Mamlaka. Aidha, tunawakumbusha wadau wote waliomaliza usajili wao kwa mwaka 2024 pamoja na wadau wapya, kutuma maombi ya kujisajili upya. Usajili huu ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha usimamizi na maendeleo ya sekta ya nafaka na mazao mchanganyiko nchini;

      2. Mahitaji muhimu ya usajili ni kama yanavyoonekana katika Jedwali:

Usajili kwa Watu Binafsi

Usajili kwa Makampuni

Leseni Halali ya Biashara

Leseni Halali ya Biashara

Cheti cha Mlipa Kodi (TIN)

Cheti cha Mlipa Kodi (TIN)

Cheti cha Usajili (Certificate of Registration)

Cheti cha Usajili (Certificate of Incorporation)

Cheti cha Usafishaji wa Kodi (Tax Clearance)

Cheti cha Usafishaji wa Kodi (Tax Clearance)

Kitambulisho cha Taifa (NIDA)

 

      3. Usajili utafanyika kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha https://asds.kilimo.go.tz/register;

      4. Wasafirishaji wote watapata cheti cha usajili ambacho kitakuwa ni kigezo mojawapo cha kupata Kibali cha kutoa au kuingiza ndani ya nchi pamoja na kushiriki minada ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko na kidijitali;

     5. Kwa maelezo zaidi piga simu namba +255714605155 au tembelea Tovuti www.copra.go.tz kwa taarifa zaidi.

 

Tangazo hili limetolewa na:

Irene M. Mlola

 MKURUGENZI MKUU

MAMLAKA YA UDHIBITI WA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO