TANZANIA IMESHIKA NAFASI YA PILI DUNIANI KWA UZALISHAJI WA MBAAZI

Tanzania imeshika nafasi ya pili duniani kwa uzalishaji wa Mbaazi ambapo kwa msimu wa mwaka jana imesafirisha takriban tani 350,000 kwenda nchini India. Katika Msimu wa Mwaka huu mbaazi zinazozalishwa Tanzania zinatarajiwa kuwa zaidi ya tani 400,000. Kutokana na ongezeko la uzalishaji kumepelekea kushuka kwa bei ya mbaazi duniani. Katika kuwawezesha wakulima wa zao hilo kupata soko, Serikali ya Tanzania inachukua hatua za makusudi za kufanya Mpango wa kuuza Mbaazi moja kwa moja kwenda Serikali ya India.
Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), imeongoza ujumbe wa serikali kwenda nchini India kuendeleza mazungumzo ambapo wamekutana na Katibu Mkuu wa Wizara inayosimamia masuala ya walaji na kuongelea Mpango huo wa Tanzania na utekelezaji wake.