Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Cereals and Other Produce Regulatory Authority

(COPRA)

COPRA Logo
"Commercialization of the Tanzania’s Food systems to catalyze growth and resilience"

SERIKALI INATARAJIA KUONGEZA IDADI YA WAKULIMA PAMOJA NA ENEO LA UZALISHAJI WA ZAO LA KAKAO NCHINI

Reason Image

Kauli hiyo imetolewa tarehe 25 Aprili 2025 na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), Bi. Irene Mlola, mara baada ya kusaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) na taasisi ya Corus International kwa ajili ya kushirikiana katika kuendeleza tasnia ya zao la kakao.

Bi. Mlola amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu zilizopo, wakulima wa kakao nchini Tanzania ni zaidi ya laki moja (100,000), ambao wengi wao wanapatikana katika mikoa ya Mbeya, Morogoro na Tanga. Aidha, amesisitiza kuwa serikali kupitia COPRA itaongeza ufanisi katika mnyororo wa thamani wa zao la kakao kwa kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora zitakazowawezesha kuongeza uzalishaji na kupata bei nzuri katika soko la dunia.

Kuhusu kuongeza uzalishaji, Bi. Mlola amesema kuwa lengo la serikali ni kuongeza uzalishaji wa kakao kutoka tani 14,000 za sasa hadi kufikia tani 30,000 ifikapo mwaka 2030, na kuongeza thamani ya mauzo kutoka dola za Marekani milioni 89 hadi zaidi ya dola milioni 200, kupitia matumizi ya mfumo wa Stakabadhi za Ghala na Minada ya Kidijitali.

Makubaliano kati ya COPRA na Corus International yanalenga pia kushirikiana katika kuhakikisha uzalishaji unazingatia viwango na kanuni za kimataifa ili kuwanufaisha wakulima na kuwawezesha kupata fursa katika soko la Ulaya.