Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) imekutana Jijini Arusha kwa siku tatu kwa ajili ya Kikao cha Menejimenti cha kutafakari masuala mbalimbali ya Taasis
Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) imekutana Jijini Arusha kwa siku tatu kwa ajili ya Kikao cha Menejimenti cha kutafakari masuala mbalimbali ya Taasis

Kuanzia tarehe 02/12/2024 mpaka tarehe 04/12/2024 Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) ikiongozwa na Mkurugenzi wake Mkuu, Bi. Irene M. Mlola imekutana Jijini Arusha kwa siku tatu kwa ajili ya Kikao cha Menejimenti cha kutafakari masuala mbalimbali ya Taasisi (Management Retreat) ikiwa ni pamoja na kujadili changamoto ilizokutana nazo wakati wa utejelezaji wa majukumu ya Mamlaka kwa robo ya kwanza ya mwaka 2024-2025, kusikia na kujadili dira ya kila Idara na Kitengo pamoja na malengo iliyojiwekea kwa kipindi cha miezi sita na miaka miwili ijayo mpaka kufikia June 2026. Vilevile, kikao hicho kilitumika kama jukwaa maalum la kujenga mahusiano baina ya viongozi wa Mamlaka (team building).