Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Cereals and Other Produce Regulatory Authority

(COPRA)

COPRA Logo
"Commercialization of the Tanzania’s Food systems to catalyze growth and resilience"

SERIKALI NA WADAU WAWEKA MIKAKATI KUONGEZA UZALISHAJI WA KAKAO HADI TANI ELFU 80.

Reason Image

Kikao cha wadau wa zao la kakao kimeazimia kuongeza uzalishaji wa zao hilo hadi kufikia tani elfu 80 mwaka 2030.

Katika kikao hicho kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Beno Malisa, wadau hao wameazimia kuweka mikakati na kuitekeleza kwa kushirikiana ili kufikia lengo hilo.

Miongoni mwa mikakati hito ni upatikanaji wa miche bora pamoja na huduma za ugani kwa wakulima wa kakao nchi nzima.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) Bi. Irene Mlola COPRA Tanzania itazalisha tani elfu themanini za kakao iifikapo mwaka 2030 kwa kuwasimamia vizuri wakulima wa zao hilo kwa kuwapatia pembejeo na huduma za ugani.

Mkurugenzi Mkuu Mlola amesema hadi sasa wakulima wa Tanzania wanazalisha Tani kumi na saba (17) za kakao kwa mwaka kiasi ambacho ni kidogo ikilinganishwa na fursa kubwa ya uzalishaji iliyopo katika mikoa yote inayozalisha zao hilo hapa nchini.