Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Cereals and Other Produce Regulatory Authority

(COPRA)

COPRA Logo
"Commercialization of the Tanzania’s Food systems to catalyze growth and resilience"

π‚πŽππ‘π€ π˜π€π–π€ππŽπ€ π–π€π•π”ππ€π‰πˆ ππ€π‘π€π‚π‡πˆπ‚π‡πˆ πŠπ”π‹πˆππƒπ€ π”ππŽπ‘π€ 𝐖𝐀 πŒπ€π™π€πŽ

Reason Image

Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) imewapatia mafunzo maalum ya siku mbili wavunaji wa parachichi kutoka Nyanda za Juu Kusini, kwa lengo la kuboresha mbinu za uvunaji na kuhifadhi ubora wa zao hilo linalozidi kuimarika katika soko la kimataifa.

Mafunzo hayo yaliyofanyika Machi 03–04, 2026 yaliwakutanisha wataalamu, wakulima na wasimamizi wa mashamba kujadili viwango vya soko la nje.

Mkurugenzi wa Mazao ya Bustani na Pareto wa COPRA, Lilian Mpinga, alisema juhudi hizo ni sehemu ya mkakati wa Serikali kukabili changamoto za mnyororo wa thamani, ikiwemo upotevu na kushuka kwa ubora wakati wa uvunaji, huku akisisitiza umuhimu wa kuwa na wavunaji wenye ujuzi na wanaotambulika rasmi.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo John Mabagala alikumbusha kuwa uvunaji sahihi huathiri uzito, ladha na muda wa kuhifadhi, hasa kwa matunda ya daraja la kwanza yanayouzwa nje. Washiriki walielekezwa kutumia vifaa vinavyofaa kama mkasi na visu safi, mifuko ya pamba na kreti badala ya viroba, pamoja na kusafisha vifaa kwa spirit ili kuzuia maambukizi.

Aidha, COPRA inaanzisha vituo rasmi vya kukusanyia parachichi ili wanunuzi watumie vituo hivyo badala ya kwenda mashambani, hatua inayolenga kulinda hadhi ya parachichi ya Tanzania katika soko la dunia ambako ubora ni msingi wa ushindani.