SERIKALI YAZINDUA NDEGE NYUKI (DRONES)
SERIKALI YAZINDUA NDEGE NYUKI (DRONES)
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) amezindua ndege nyuki (drones) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Afrika wa Matumizi Endelevu ya Zana za Kilimo, unaofanyika tarehe 3 Februari 2026 katika Hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam.
Ndege nyuki hizo zimekabidhiwa kwa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) kwa kushirikiana na Bodi ya Korosho; Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA); na Idara ya Zana za Kilimo iliyopo Wizara ya Kilimo.
Viongozi walioshuhudia Uzinduzi huo ni pamoja na Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli; na Mha. Athumani J. Kilundumya, Naibu Katibu Mkuu (Umwagiliaji na Zana za Kilimo).
