Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Cereals and Other Produce Regulatory Authority

(COPRA)

COPRA Logo
"Commercialization of the Tanzania’s Food systems to catalyze growth and resilience"

SERIKALI YAHIMIZA ULINZI WA AFYA YA MIMEA KUIMARISHA USALAMA BIASHARA YA MAZAO

Reason Image

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb), amesema ulinzi wa afya ya mimea una nafasi muhimu katika kuimarisha usalama wa chakula, kuongeza ushindani wa mazao ya Tanzania kibiashara kwenye masoko ya kikanda na kimataifa.

COPRA imeshiriki Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Afya ya Mimea yaliyofanyika Dodoma kama sehemu ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano na taasisi mbalimbali katika kusimamia biashara ya mazao inayozingatia viwango, ubora na mifumo rasmi ya biashara.

Kupitia ushirikiano huu, Tanzania inaimarisha uaminifu wa mazao yake kwenye masoko, kulinda maslahi ya wadau kwenye mnyororo wa thamani wa mazao na kuendeleza mikakati ya Taifa ya kujenga sekta ya kilimo yenye ushindani, tija na biashara salama ya mazao.