Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Cereals and Other Produce Regulatory Authority

(COPRA)

COPRA Logo
"Commercialization of the Tanzania’s Food systems to catalyze growth and resilience"

COPRA YACHAGIZA KILIMO KIBIASHARA TABORA

Reason Image

Je, unajua juhudi za Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) zinavyoendelea kubadili mwelekeo wa kilimo biashara Mkoani Tabora?

 

Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Mhe. Gerald Mongella ameipongeza COPRA kwa mchango wake katika kuchagiza kilimo kibiashara, akisisitiza umuhimu wa kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa elimu sahihi, hasa kuhusu masoko ya mazao kupitia mifumo ya kidijitali.

 

📈 Matokeo yanaonekana:

* Bei ya choroko imeongezeka kutoka Tsh 600–700 hadi Tsh 1400–1550 kupitia minada ya kidijitali

* Zaidi ya kilo 1,700 za mbegu bora za choroko na mbaazi zimesambazwa kwa wakulima

* Maafisa ugani 94 wamepatiwa mafunzo ili kuwafikia wakulima hadi ngazi ya vijiji

 

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kanda ya Magharibi, Gilbert Nzunda, jitihada zinaendelea kuingiza mazao mengine kama karanga, ufuta na mbaazi kwenye mfumo wa stakabadhi ghalani katika Mkoa wa Tabora ili kuongeza tija na ushindani wa soko.

Katika maonesho hayo wakati wa kuadhimisha wiki ya Ushirika, wito umetolewa kuongeza ubunifu kwenye maonesho ili wananchi wengi zaidi wapate elimu na kunufaika na fursa zilizopo.

 

Kilimo kibiashara kinaanza na taarifa sahihi na masoko yenye uwazi.