Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Cereals and Other Produce Regulatory Authority

(COPRA)

COPRA Logo
"Commercialization of the Tanzania’s Food systems to catalyze growth and resilience"

KILO 9,400 ZA MBEGU BORA YA ALIZETI KUONGEZA UZALISHAJI WA ZAO HILO GEITA

Reason Image

Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) mekabidhi tani 94 za mbegu bora za alizeti kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela.

 

Hatua hii ya kimkakati ya Serikali katika kuimarisha uzalishaji wa zao la Alizeti ili kuongeza upatikanaji wa mafuta ya kula nchini.

 

Akizungumza baada ya kupokea mbegu hizo Mhe. Shigela amesema mpango huo ni kichocheo muhimu cha kuongeza tija ya uzalishaji, kuinua kipato cha wakulima na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa mkoa wa Geita na Taifa kwa ujumla.

 

Mkurugenzi Mkuu wa COPRA Bi. Irene Mlola alisema kuwa ugawaji wa mbegu hizo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokutana na wananchi wa Geita mwezi Oktoba 2025.

 

Aliongeza kuwa, matumizi sahihi ya mbegu bora za alizeti ni hatua ya msingi katika kuimarisha mnyororo wa thamani wa zao hilo ili kukidhi mahitaji ya viwanda vya ndani na kupunguza utegemezi wa uagizaji wa mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.

 

Aidha Mkurugenzi Mkuu Mlola amesisitiza kuwa COPRA itaendelea kusimamia uzalishaji, ubora na masoko ya zao la alizeti kwa uwazi na weledi ili kuhakikisha wakulima wananufaika, viwanda vinapata malighafi ya uhakika na Taifa linaimarisha uzalishaji wa ndani.