COPRA YATAMBULISHA MFUMO WA COPRA-MIS KWA WADAU
Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) imeendesha mafunzo maalumu ya matumizi ya mfumo wa taarifa unaofahamika kama COPRA-MIS kwa zaidi ya wadau 100 wakiwemo vijana wa BBT-Ugani 82, wazabuni wa pembejeo za kilimo 8 na Wakuu wa Divisheni ya Kilimo kwenye halmashuri 16 za mikoa ya Nyanda za Juu Kusini,
Mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Mbeya yamelenga kuwafundisha washiriki namna ya kuingiza taaifa za wadau ili kuanza kwa zoezi la kuwasajili kwenye mfumo huo wadau wote wanaohusika na mnyororo wa thamani wa zao la parachichi wakiwemo wakulima, wauzaji wa mbegu na miche, wauzaji wa pembejeo na wadau wengine wote.
Matumizi ya mfumo wa kidijitali wa COPRA-MIS ni juhudi za serikali kuhakikisha kuwa shughuli za kilimo zinarasimishwa ili ziweze kuleta tija na kuwa faida kwa wadau wanaohusika huku zikiingiza kipato kwa wahusika na kuongeza mauzo kwenye soko la ndani na lile la kimataifa.
