Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Cereals and Other Produce Regulatory Authority

(COPRA)

COPRA Logo
"Commercialization of the Tanzania’s Food systems to catalyze growth and resilience"

COPRA NA TBS: VIWANGO VIPYA KUIMARISHA UBORA NA UENDELEVU WA UZALISHAJI WA MAZAO

Reason Image

COPRA kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), imeandaa rasimu za viwango vya kwanza nchini vya Kanuni Bora za Kilimo (GAP) kwa uzalishaji endelevu wa nafaka, mikunde na mazao ya bustani/hotikacha.

Viwango hivi vinalenga:
✅ Kuongeza uzalishaji na tija.
✅ Kuimarisha ubora na usalama wa mazao.
✅ Kulinda mazingira, rutuba ya udongo na afya za wakulima.
✅ Kuongeza ushindani wa mazao ya Tanzania katika masoko ya ndani na kimataifa.

📢 MAONI YAKO NI MUHIMU!
Wadau wa kilimo wanahimizwa kupitia rasimu hizo na kutoa maoni na mapendekezo yao kupitia njia zifuatazo:
🌐 Tovuti: <Link url="https://www.copra.go.tz/" title="www.copra.go.tz"/>
📧 Barua pepe: info@copra.go.tz
📅 Mwisho wa kupokea maoni: 15 Oktoba 2026.

Aidha, kupitia kanda zake saba nchini, COPRA inaendelea kuratibu zoezi la Mapitio ya Umma kwa kuwapa wadau fursa ya kutoa maoni na mapendekezo yatakayochangia kukamilisha viwango hivyo kwa kuzingatia uhalisia wa shughuli za kilimo katika maeneo mbalimbali ya nchi.