Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Cereals and Other Produce Regulatory Authority

(COPRA)

COPRA Logo
"Commercialization of the Tanzania’s Food systems to catalyze growth and resilience"

KILIMANJARO NA MBEYA WATOA MAONI KUBORESHA VIWANGO VYA KILIMO ENDELEVU

Reason Image

 

Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), imeendelea kushirikisha wadau wa sekta ya kilimo katika mapitio ya rasimu za Kanuni Bora za Kilimo (GAP) kwa uzalishaji endelevu wa mazao ya bustani, nafaka na mikunde.

Kupitia vikao vya kupokea maoni, wadau wameonesha matumaini kuwa viwango hivyo vitachangia kuongeza tija na ubora wa mazao, kuimarisha usalama wa wazalishaji na walaji, kulinda mazingira na kuongeza ushindani wa mazao ya Tanzania katika masoko ya ndani na nje ya nchi. Wadau pia wameeleza matarajio yao ya kuona viwango hivyo vinatekelezwa kwa manufaa ya wakulima na biashara ya mazao.

Vikao vya kupokea maoni ya wadau vimefanyika jijini Mbeya kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na mjini Moshi kwa Kanda ya Kaskazini huku mchakato ukiendelea katika kanda mbalimbali nchini ili kuhakikisha viwango vinazingatia maoni ya wadau na mazingira halisi ya uzalishaji.