Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Cereals and Other Produce Regulatory Authority

(COPRA)

COPRA Logo
"Commercialization of the Tanzania’s Food systems to catalyze growth and resilience"

COPRA YAKABIDHI MBEGU BORA KUIMARISHA UZALISHAJI

Reason Image

Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) imekabidhi mbegu ya choroko kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kwa lengo la kugawiwa bure kwa wakulima. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Uendeshaji na Udhibiti Ubora wa COPRA, Bw. Kamwesige Mtembei, amesema kuwa mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na wakulima katika kila hatua ya uzalishaji hadi kufikia masoko ili kuhakikisha wanapata tija na faida katika shughuli zao za kilimo.

Kwa upande wake, Mhe. Anamringi Macha ameeeleza kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuunga mkono juhudi za wakulima kwa kuhakikisha wanazalisha kwa ufanisi na kuuza mazao yao kwa uwazi na kusisitiza umuhimu wa kuunda vyama imara vya ushirika kama njia ya kuwawezesha wakulima kufanya maamuzi huru na kuuza mazao yao kwa haki, hivyo kuongeza kipato na maendeleo ya sekta ya kilimo mkoani Simiyu.