COPRA YAANZA SAFARI URASIMISHAJI BIASHARA YA MAHINDI
Biashara ya mahindi mkoani Rukwa inaingia hatua mpya, Serikali kupitia COPRA ikichochea ujenzi wa mfumo rasmi, wenye uwazi na ushindani zaidi kwa manufaa ya wakulima, wafanyabiashara na wadau wa mnyororo wa thamani.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Makongoro Nyerere, Julai 28, 2026 ameongoza mkutano wa wadau wa zao la mahindi mjini Sumbawanga, uliowakutanisha COPRA, taasisi za Serikali kama vile TMX, WRRB, TCDC, sekta binafsi, wakulima na wafanyabiashara kuweka msingi wa maboresho ya biashara ya zao hilo.
Hatua zinazofuata zitalenga kuimarisha huduma za maghala, biashara ya kidijitali, vyama vya ushirika, upatikanaji wa huduma za kifedha na kuwaunganisha wakulima na masoko mengi zaidi ya ndani na nje ya nchi.
Lengo ni moja: Mahindi yenye soko, mkulima mwenye fursa, na biashara yenye ushindani.
