COPRA YAINGIA MAKUBALIANO YA KIMKAKATI NA YAS BUSINESS NA MIXX BY YAS

Leo tarehe 9 Julai, COPRA imesaini makubaliano ya kimkakati na Yas Business pamoja na MIXX by Yas, kwa lengo la kuimarisha matumizi ya mifumo ya kidigitali katika upatikanaji wa masoko, taarifa sahihi za bei ya mazao, malipo, na huduma nyingine za kifedha kwa wakulima na wadau katika mnyororo wa thamani wa mazao ya nafaka na mazao mchanganyiko.
Makubaliano haya ni sehemu ya jitihada za COPRA za kukuza uwazi wa soko, kuongeza ufanisi katika biashara ya mazao, na kuwezesha wakulima kupata huduma kwa njia ya haraka na salama kupitia teknolojia.
Mkataba huu umesainiwa na:
• Bi. Angelica Pesha – Afisa Mtendaji Mkuu, MIXX by Yas
• Bi. Irene M. Mlola – Mkurugenzi Mkuu, COPRA
• Bw. James Sumari – Mkurugenzi wa Biashara, MIXX by Yas
Tunatarajia ushirikiano huu utaongeza thamani katika utekelezaji wa majukumu ya COPRA kwa kuhakikisha wakulima na wadau wote wanapata huduma za soko na taarifa muhimu kwa wakati, kwa njia shirikishi na endelevu.