Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Cereals and Other Produce Regulatory Authority

(COPRA)

COPRA Logo
"Commercialization of the Tanzania’s Food systems to catalyze growth and resilience"

COPRA YAONGEZA NGUVU UZALISHAJI MBEGU BORA

Reason Image

Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) imeendelea na juhudi za kukabiliana na changamoto ya upatikanaji mdogo wa mbegu bora kwa mazao mbalimbali.

Juhudi hizo zimeonekana kwa COPRA kufanikisha mafunzo ya kuzalisha mbegu kwa wakulima wa mkoa wa Singida yaliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Itigi Mhe. Hussein Simba ameipongeza COPRA kwa juhudi za kuimarisha sekta ya kilimo pamoja na kuijumuisha Halmashauri ya Itigi kwenye mipango hiyo.

Aidha, ameiomba COPRA kusaidia kupatikana kwa maghala ya kuhifadhia mazao jambo linalowasabibishia wakulima Kwenda umbali mkubwa kutafuta huduma.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji wa Mkoa wa Singida Stanslaus Choaji amewataka wakulima kuzingatia maelekezo ya wakufunzi ili wakatekeleze kwa usahihi jukumu la kuzalisha mbegu kwani ufanisi wao utapelekea kuongeza upatikanaji wa mbegu bora kwenye maeneo yao.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao na Viwango kutoka COPRA makao makuu ametoa wito kwa vijana na wanawake kujitokeza na kuwania fursa zinazotolewa na COPRA katika kilimo huku akisisitiza kuwa kilimo kinalipa n ani chanzo cha kuaminika cha ajira na kipato.

Wakulima 35 wanashiriki mafunzo ya kuzalisha mbegu yanayoendeshwa na TOSCI kwa ufadhili wa COPRA wakipatiwa kilo 4,000 za mbegu mama ya dengu inayotarajiwa kutoa kilo 40,000 baada ya uzalishaji ikiwa ni juhudi za serikali kutatua changamoto ya upungufu wa mbegu bora nchini.