Kikao cha Wadau wa Mpango wa Pamoja wa Mbegu (JSAP) - Morogoro
Kikao Kazi cha Uandishi ya Mpango wa Pamoja wa Mbegu (JSAP) wa Mazao ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, kimefanyika Morogoro kuanzia tarehe 06 Novemba 2024 na kuhitimishwa tarehe 08 Novemba 2024 kwa kujumuika na wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi.
Viongozi kutoka maeneo mbalimbali kama Wizara ya Kilimo, COPRA, TOSCI, TASTA, TASEPA, SUA, Kamati ya Uzalishaji Mbegu, Commercial Growers Association, TOAM, Kilimo Maendeleo, AYEGRO, na wengine wengi wamekutana ili kuandaa mpango utakaoboresha sekta ya mbegu Tanzania haswa eneo la nafaka na mazao mchanganyiko
Lengo la kikao kazi hiki ni pamoja na: -
1. Kupitia rasimu ya JSAP ili kuimarisha ubora, usambazaji na upatikanaji wa mbegu;
2. Kuweka wazi majukumu ya taasisi zote kwenye mnyororo wa mbegu; na
3. Kuimarisha ushirikiano kwa kilimo endelevu, usalama wa chakula na ukuaji wa kiuchumi.
JSAP inatupeleka kwenye njia ya kuongeza tija, masoko, kuwawezesha wakulima, na kuhakikisha upatikanaji wa mbegu bora kwa wote