Tanzania Imevuka Lengo Mauzo ya Nje Parachichi
Tanzania Imevuka Lengo Mauzo ya Nje Parachichi
Tanzania imevuka lengo la kitaifa la mauzo ya nje ya parachichi la tani 40,000 lililowekwa kufikiwa mwaka 2030, baada ya mauzo ya nje ya zao hilo kufikia tani 52,000 mwaka 2025/2026, ikiwa ni ongezeko la asilimia 237 kutoka tani 15,432.77 mwaka 2020/2021.
Mafanikio hayo yameenda sambamba na ongezeko la mapato ya fedha za kigeni kutoka Dola za Marekani milioni 44.2 mwaka 2020/2021 hadi milioni 97.2 mwaka 2025/2026, sawa na ongezeko la asilimia 120.4, huku uzalishaji ukiongezeka kutoka tani 149,340 hadi tani 203,473, sawa na ongezeko la asilimia 36.24.
