Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Cereals and Other Produce Regulatory Authority

(COPRA)

COPRA Logo
"Commercialization of the Tanzania’s Food systems to catalyze growth and resilience"

TANZANIA IMEUZA TANI MILIONI 23.4 ZA CHOROKO KATIKA MSIMU WA KILIMO 2025/2026

Reason Image

Akizungumza kwenye mkutano wa ufunguzi wa msimu wa mauzo ya zao la choroko wa mwaka 2026/2027, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), Irene Mlola amesema tani hizo za choroko zimeuzwa kupitia mifumo rasmi ya stakabadhi za ghala na minada ya kidigitali


Mkurugenzi Mkuu Mlola amesema mafanikio hayo ya urasimishaji wa biashara ya mazao ni matokeo ya ushirikiano kati ya COPRA, Tawala za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wakulima na wadau wengine ambao umewezesha wakulima kufanya biashara kwa haki na uwazi na serikali kupata takwimu za uzalishaji zinazowezesha kuweka mipango ya maendeleo ya mazao kuanzia uzalishaji hadi mnyororo wa biashara.