Mkutano wa kwanza wa wadau wa mashauriano kuhusu utekelezaji wa Kanuni za Sheria ya Usalama wa Chakula (Cap. 249) na marekebisho ya Sheria ya Nafaka na Mazao Mengine (Cap. 274) - Desemba 2024

Mkutano wa kwanza wa mashauriano kuhusu utekelezaji wa Kanuni za Sheria ya Usalama wa Chakula (Cap. 249) na marekebisho ya Sheria ya Nafaka na Mazao Mengine (Cap. 274) ulifanyika tarehe 6 Desemba jijini Dar es Salaam!
Mkutano huu uliwalenga wadau wa sekta binafsi, kama vile NGOs, washirika wa maendeleo, na wafadhili, kwa lengo la kushirikiana kuimarisha mifumo ya usalama wa chakula na kuboresha maisha ya wakulima na wadau wote wa mnyororo wa thamani wa mazao yanayosimamiwa na COPRA. Mazao haya yamegawanywa katika makundi yafuatayo:
1. Nafaka
2. Mbegu za mafuta na karanga
3. Mazao ya bustani (matunda, mbogamboga, viungo, maua, na vikolezo)
4. Mazao jamii ya mikunde
5. Mazao ya mizizi
Huu ni mwanzo wa mfululizo wa vikao vya kikanda ambavyo vitawalenga wadau wengine wa mnyororo wa thamani katika maeneo mbalimbali ya Tanzania mwezi huu wa Desemba.
Tunatoa shukrani za dhati kwa mshirika wetu @amdttz kwa mchango wao mkubwa kufanikisha mkutano huu.
#ShirikishaBoreshaEndeleza #UsalamaWaChakula #COPRA